Thursday, 10 December 2015

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI WA MAGUFULI

HOTUBA YA JPM KUTANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI.
Magufuli: Ndugu waandishi wa habari na watanzania kwa ujumla, ninawasalimu sana. Nawakaribisha katika kikao hiki cha kutangaza baraza la mawaziri,
Tutakuwa na mawaziri 19, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama.
Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elekezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure.
Wizara ni 18 lakini Mawaziri ni 19 kwa sababu wizara ya Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma naiunganisha na Utawala bora na TAMISEMI hivyo itakua na mawaziri wawili. Wizara ni kama ifuatavyo;
1. Ofisi ya Rais, Tamesemi utumishi na utawala bora,
-MAWAZIRI; Simbachawene na Kairuki,
-NAIBU; Selemani Jaffo
2. Muungano na Mazingira:
-WAZIRI; January Makamba,
-NAIBU; Luhaga Mpina
3. Ajira, walemavu:
-WAZIRI; Jenista Mhagama,
-MANAIBU; nimemtua mbunge, Abdalah Posi Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma na Anthonu Mavunde,
4. Mambo ya Ndani,
-WAZIRI; Charless Kitwanga,
-NAIBU; Bado
5. Kilimo, mifugo na uvuvi:
-WAZIRI; Mwigulu Nchemba,
-NAIBU; Willium Nashe
6. Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano:
-WAZIRI; Waziri bado sijamtafuta,
-NAIBU; Edwin Ngonyani.
7. Fedha na Mipango:
-WAZIRI; bado,
-NAIBU; Ashanyi Kijaji
8. Nishati na madini:
-WAZIRI; Sospeter Muhongo,
-NAIBU; Medadi
9. Katiba na sheria:
-WAZIRI; Mwakyembe,
-NAIBU bado
10. Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki:
-WAZIRI; Augustino Mahiga nimemteua mbunge na waziri,
-NAIBU; Dr.Suzan Kolimba,
11. Ulinzi na JKT:
-WAZIRI; Dr. Hussein Mwinyi,
NAIBU; bado
12. Ardhi na maendeleo ya makazi:
-WAZIRI; Wiliam Lukuvi,
-NAIBU; Angelina Mabula
13. Utalii:
-WAZIRI; bado
-NAIBU; Makanye
14. Viwanda, Biashara na Uwekezaji:
-WAZIRI; Charles Mwijage
-NAIBU; Bado
15. Elimu, Sayansi na mafunzo ya ufundi:
-WAZIRI; Waziri bado,
-NAIBU; Stella Manyanya
16. Afya na Ustawi wa jamii:
WAZIRI; Ummy Mwalimu,
NAIBU; Hamis Kingwangala
17. Habari, Utamaduni na Michezo:
-WAZIRI; Nape Nnauye,
-NAIBU; Wambura
18. Maji na umwagiliaji:
-WAZIRI; Makame Mbarawa,
-NAIBU; Kamwele

Tuesday, 8 December 2015

#CRDB chanika yavamiwa na majambazi



‪#‎Habari‬ Majambazi wamevamia na kupora pesa CRDB na DCB Bank Chanika na kuua kwa risasi watu 2 na kujeruhi baadhi ya wafanyakazi. kwa taarifa zaidi endelea kutufatilia taarifa zetu.