Sunday, 22 February 2015

MKUU WA KITUO CHA POLISI NJOMBE MlAKA 30 JELA KWA KUBAKA

Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilembula
Njombe Afungwa Jela Miaka 30
kwa kosa la Kumbaka Mahabusu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa
ya Njombe, imemhukumu aliyekuwa
mkuu wa kituo cha Polisi Ilembula
kifungo cha miaka 30 jela, baada
ya kukutwa na hatia ya kumbaka
mtuhumiwa aliyekuwa ndani ya
mahabusu.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu
Augustine Rwezile, baada ya
mshtakiwa huyo James Nyambenga
kukiri kosa hilo mahakamani,
ambapo mshakiwa huyo anadaiwa
kumtoa msichana huyo kwenye
chumba cha mahabusu alikokuwa
anashikiliwa na kumbaka.
Mwanamke huyo ambae ni
mhudumu wa bar alikuwa
anashikiliwa kwenye mahabusu ya
kituo hicho kwa tuhuma za
uzururaji.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu
Rwezile amesema ushahidi
uliotolewa na upande wa
mlalamikaji na vielelezo vya daktari
aliyempima msichana huyo viliweza
kuithibitishia Mahakama kuwa
mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

1 comment: