Sunday, 22 February 2015

MARIE STOPES YATENGA BILIONI 37.2 KWAAJILI YA MIRADI YA UZAZI MIKOA MINNE

Marie Stopes Tanzania yatenga Bilioni 37.2 kushughulikia miradi ya uzazi mikoa ya minne
23 February 2015 By dewjiblog 0 comments

Kaimu Mkurugenzi wa Marie Stopes Tanzania, Mwemezi Ngemera akizungumza na wakazi wa Ilongero kuhusu huduma za Mkoba za Uzazi wa Mpango.

Na Nathaniel Limu, Singida

SHIRIKA  lisilo la kiserikali la Marie Stopes Tanzania (MST) linatarajia kutumia zaidi ya shilingi 37.2 bilioni (Pounds 14  milioni), kugharamia mradi wa uzazi wa mpango wa uzazi wa mpango na elimu ya afya ya uzazi kwa vijana  utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mine kuanzia sasa katika mikoa ya Singida, Kilimanjaro, Manyara na Katavi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Marie Stopes Tanzania, Mwemezi Ngemera, wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma za mkoba za uzazi wa mpango uliofanyika kimkoa katika kijiji cha Ilongero Wilaya ya Singida.

Alisema fedha hizo zimetolewa na  kufadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la UKAID. Ufadhili huo utaliwezesha shirika  la MST kutoa bure huduma za njia mbalimbali za uzazi wa mpango kupitia huduma za Mkoba ( outreach services).

Mrembo anayeshikilia taji la Miss Marie Stopes Doreen Benne akiwashauri vijana wa Ilongero Mkoani Singida kutumia njia za uzazi wa mpango.

Ngemera alisema malengo yao ni kumwezesha kila mtu kuchagua njia ya uzazi wa mpango anayoihitaji hasa miongoni mwa vijana.

“ Vijana wanaweza kudhani kuwa huduma za uzazi wa mpango ni kwa ajili ya watu walio katika ndoa tu, lakini ni muhimu pia kwao ili kuzuia mimba zisizo takiwa kabla ya ndoa. Nawaomba vijana kuhamasika na kampeni yetu ya chagua maisha kwa kutumia uzazi wa mpango”,alifafanua.

Kwa upande wake Miss Marie Stopes 2014, Doreen Benne, alisema mimba ambazo hazijapangiliwa, huchangia takribani vifo 1,400 kila mwaka vitokanavyo na utoaji mimba usiosalama.

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali Mkoani Singida wakisikiliza huduma za uzazi wa  mpango.

Pia zinachangia mamia ya wasichana kufukuzwa shule kwa kuwa na mimba zisizotarajiwa.

Alisema hatari ya hizo au madhara hayo yanaweza kutokomezwa /kuzuiwa endapo kila mtu atazingatia kikamilifu uzazi wa mpango.

Shirika la Marie Stopes ambalo mwaka jana lilishafikia miaka 25 kufanya kazi nchini, linahudumia na kuchangia asilimia 25 ya huduma za uzazi wa mpango unaotekelezwa hapa nchini.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida Wilbard Marandu akikata utepe wakati wa kuzindua gari litakalotumika kutoa huduma za mkoba za uzazi wa mpango Mkoani Singida.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida Wilbard Marandu akizindua gari litakalotumika kutoa huduma za mkoba za uzazi wa mpango Mkoani Singid

No comments:

Post a Comment