Thursday, 10 December 2015

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI WA MAGUFULI

HOTUBA YA JPM KUTANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI.
Magufuli: Ndugu waandishi wa habari na watanzania kwa ujumla, ninawasalimu sana. Nawakaribisha katika kikao hiki cha kutangaza baraza la mawaziri,
Tutakuwa na mawaziri 19, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama.
Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elekezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure.
Wizara ni 18 lakini Mawaziri ni 19 kwa sababu wizara ya Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma naiunganisha na Utawala bora na TAMISEMI hivyo itakua na mawaziri wawili. Wizara ni kama ifuatavyo;
1. Ofisi ya Rais, Tamesemi utumishi na utawala bora,
-MAWAZIRI; Simbachawene na Kairuki,
-NAIBU; Selemani Jaffo
2. Muungano na Mazingira:
-WAZIRI; January Makamba,
-NAIBU; Luhaga Mpina
3. Ajira, walemavu:
-WAZIRI; Jenista Mhagama,
-MANAIBU; nimemtua mbunge, Abdalah Posi Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma na Anthonu Mavunde,
4. Mambo ya Ndani,
-WAZIRI; Charless Kitwanga,
-NAIBU; Bado
5. Kilimo, mifugo na uvuvi:
-WAZIRI; Mwigulu Nchemba,
-NAIBU; Willium Nashe
6. Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano:
-WAZIRI; Waziri bado sijamtafuta,
-NAIBU; Edwin Ngonyani.
7. Fedha na Mipango:
-WAZIRI; bado,
-NAIBU; Ashanyi Kijaji
8. Nishati na madini:
-WAZIRI; Sospeter Muhongo,
-NAIBU; Medadi
9. Katiba na sheria:
-WAZIRI; Mwakyembe,
-NAIBU bado
10. Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki:
-WAZIRI; Augustino Mahiga nimemteua mbunge na waziri,
-NAIBU; Dr.Suzan Kolimba,
11. Ulinzi na JKT:
-WAZIRI; Dr. Hussein Mwinyi,
NAIBU; bado
12. Ardhi na maendeleo ya makazi:
-WAZIRI; Wiliam Lukuvi,
-NAIBU; Angelina Mabula
13. Utalii:
-WAZIRI; bado
-NAIBU; Makanye
14. Viwanda, Biashara na Uwekezaji:
-WAZIRI; Charles Mwijage
-NAIBU; Bado
15. Elimu, Sayansi na mafunzo ya ufundi:
-WAZIRI; Waziri bado,
-NAIBU; Stella Manyanya
16. Afya na Ustawi wa jamii:
WAZIRI; Ummy Mwalimu,
NAIBU; Hamis Kingwangala
17. Habari, Utamaduni na Michezo:
-WAZIRI; Nape Nnauye,
-NAIBU; Wambura
18. Maji na umwagiliaji:
-WAZIRI; Makame Mbarawa,
-NAIBU; Kamwele

Tuesday, 8 December 2015

#CRDB chanika yavamiwa na majambazi



‪#‎Habari‬ Majambazi wamevamia na kupora pesa CRDB na DCB Bank Chanika na kuua kwa risasi watu 2 na kujeruhi baadhi ya wafanyakazi. kwa taarifa zaidi endelea kutufatilia taarifa zetu.












Thursday, 26 November 2015

MAGUFULI KIBOKO HIVI NDIVYO MABASI YA UDA,DUKA LA SAPNA NA GARI LA BOSS WA SAPNA YALIVYO FUNGIWA KISA KUTOLIPA KODI.


TRA yaanza kung’ata, wafunga Sapna, wakamata magari UDA
MAMLAKA ya Mapato
Tanzania(TRA), imeanza
operesheni maalumu ya
kunasa wafanyabishara wakubwa
ambao wengine ni wadaiwa sugu
ambapo wanadaiwa na mamlaka hiyo
huku wafanyabishara wa duka la simu
la Sapna lililopo eneo la Posta mpya
jijini Dar es Salaam likitiwa kufuli.
Operesheni ya TRA dhidi ya
wanaodaiwa fedha ilianza jana maeneo
mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam
ambapo maofisa wa mamlaka hiyo
walikuwa wanakwenda eneo moja hadi
jingine na kote ambako wamekwenda
wamefunga ofisi za wafanyabishara
hao.
Maofisa wa TRA waliokuwa
na nyaraka mbalimbali za madeni
walipokuwa wanafika kwenye maeneo
ya wafanyabishara hao hawakuwa na
muda wa kupoteza zaidi ya kufunga
ofisi huku baadhi ya maofisa hao
walikuwa wakisema kuwa Hapa Kazi
Tu.
Duka la Sapna ililifungwa jana saa
tisa alasiri ambapo maofisa wa TRA
ambao hawakuwa tayari kutaja majina
yao walidai kuwa wamiliki wa duka
hilo ni miongoni mwa wanaodaiwa
na TRA na tena ni kiasi kikubwa cha
fedha.Hata hivyo hawakutaja kiwango
halisi cha fedha huku wakifafanua kuwa
wamiliki wa duka hilo walipewa taarifa
mapema, hivyo hawakuvamia zaidi ya
kutumia utaratibu maalumu.
Wakati duka hilo linafungwa
wananchi walikuwa eneo hilo
walijikuta wakishangaa kuona namna
ambavyo wamiliki wa duka hilo wenye
asili ya Asia wakibaki wameshika
vichwa bila kujua la kufanya.Moafisa
wa TRA mbali ya kufunga duka hilo,
pia waliamua kufunga gari la mmoja
wa wamiliki wa duka hilo.

Mbali ya kufunga duka hilo pia
maofisa wa TRA walikwenda kwenye
ofisi za Shirika la Usari Dar es Salaam
(UDA), ambako nako wamekamata
baadhi ya magari kutokana na kudaiwa
kodi huku pia ikielezwa eneo lingine
ambalo mamlaka hiyo imefanya
operesheni ni eneo la Victoria ambapo
kuna kampuni inayohusika na uuzaji
wa redio upepo na rimoti za magari
.Kwenye eneo hilo magari manne
yamechukuliwa na TRA.
Kwa mujibu wa mmoja wa maofisa
wa TRA ni kwamba operesheni
hiyo itaendelea tena leo huku pia
ikielezwa kuna viwanda mbalimbali
ambavyo vimefungwa kwa kushindwa
kulipa kodi.Hata hivyo alipotafutwa
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa
mlipa kodi TRA Richard Kayombo
kuzungumzia operesheni hiyo
hakupatikana.




SAED KUBENEA AISHUKIA HALMASHAURI KINONDONI



Mbunge wa jimbo la Ubungo Mhe. Said Kubenea ameitaka halmashauri ya manispaa ya Kinondoni kuhakikisha fedha za ushuru zinazokusanywa katika masoko yote yaliyomo katika jimbo la Kinondoni zitumike katika kuboresha miundombinu ya masoko hayo ili kuwajengea hari ya kulipa ushuru wafanyabiashara hao



Hukumu kesi ya Marehemu Mawazo

(a) Agizo la Polisi limefutwa na mahakama kuu
(b) UKAWA wameruhusiwa na mahakama kuaga ila wajadili na polisi ni wapi wanaagia
(c) Polisi watoe ulinzi usiopitiliza mipaka ya kazi yao






MIKOPO YA MASHANGINGI


Uongozi Bunge: Fedha atakazopewa Mbunge wa kununua gari ni milioni 90, hautaongezwa kufikia milioni 130 kama baadhi ya Wabunge wanavyotaka.

-Baadhi ya wabunge walitaka wapewe milioni 130 kutokana na kupanda kwa thamani ya dola ya Marekani.







Friday, 14 August 2015

yanayoendlea mbeya muda huu





SONGWE INTERNATIONAL AIRPORT #MBEYA
UKAWA MEMBERS AND SUPPORTERS WAITING #HON_EDWARD_LOWASA