Friday, 27 February 2015

LAZARO NYALANDU AND PARLIAMENT COMMITEE ON TOURISM HOTELS

Arusha. A parliamentary committee is angered that the minister for Tourism, Mr Lazaro Nyalandu has been holding talks with hotel owners ostensibly to reach a consensus with them on what bed occupancy rates should be.

The Parliamentary Committee on Natural Resources and Tourism chairman, Mr James Lembeli, has raised the alarm over the meeting which the minister held recently in Arusha with the hoteliers.

Mr Lembeli said the committee will report the minister to the Speaker, Ms Anne Makinda, over the negotiations which he said contravened a resolution of the National Assembly that required the approved rates to be applied without delay.

The ministry’s permanent secretary, Dr Adelhem Meru, confirmed the meeting but said it yielded no fruit.

“There was no agreement... they were lamenting that the new rates are high and what we did was to receive their suggestions. The turnout at the meeting was also not good,” said Dr Meru.

Sources told me that the hotel owners are petitioning the government to pay between seven to $15 per client per night instead of the new rate between $35 and $50.

ADVERTISEMENT
Parliament was early this month told that the government was losing an average of Sh2 billion a month over failure by the ministry to gazette the new rates as contained in a court ruling last September.

Mr Nyalandu told Parliament then that the new changes would be gazzetted not later than February 15 but that has not been done.

“We’re shocked on how this ministry is operating. He (Nyalandu) was the one who made the February 15 promise but he is now negotiating with hotel owners instead of taking the right actions,” said Mr Lembeli.

“Minister Nyalandu is going against the Parliament and High Court’s ruling, he was tasked to execute the new formula and not holding a bargaining meeting. We can’t let him get away with it.”

Shadow minister for natural resources and tourism Rev Peter Msigwa said Mr Nyalandu should quit the dillydallying and gazette the new formula as soon as possible.

“Seventeen companies lodged a case against the government and the judge ruled in our favour but today the minister who is vested with the powers to execute the order is not doing so, what is this? I believe there’s more to it than sees the eye, there are many thing that we are are yet to know,” he said.

Sunday, 22 February 2015

MARIE STOPES YATENGA BILIONI 37.2 KWAAJILI YA MIRADI YA UZAZI MIKOA MINNE

Marie Stopes Tanzania yatenga Bilioni 37.2 kushughulikia miradi ya uzazi mikoa ya minne
23 February 2015 By dewjiblog 0 comments

Kaimu Mkurugenzi wa Marie Stopes Tanzania, Mwemezi Ngemera akizungumza na wakazi wa Ilongero kuhusu huduma za Mkoba za Uzazi wa Mpango.

Na Nathaniel Limu, Singida

SHIRIKA  lisilo la kiserikali la Marie Stopes Tanzania (MST) linatarajia kutumia zaidi ya shilingi 37.2 bilioni (Pounds 14  milioni), kugharamia mradi wa uzazi wa mpango wa uzazi wa mpango na elimu ya afya ya uzazi kwa vijana  utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mine kuanzia sasa katika mikoa ya Singida, Kilimanjaro, Manyara na Katavi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Marie Stopes Tanzania, Mwemezi Ngemera, wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma za mkoba za uzazi wa mpango uliofanyika kimkoa katika kijiji cha Ilongero Wilaya ya Singida.

Alisema fedha hizo zimetolewa na  kufadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la UKAID. Ufadhili huo utaliwezesha shirika  la MST kutoa bure huduma za njia mbalimbali za uzazi wa mpango kupitia huduma za Mkoba ( outreach services).

Mrembo anayeshikilia taji la Miss Marie Stopes Doreen Benne akiwashauri vijana wa Ilongero Mkoani Singida kutumia njia za uzazi wa mpango.

Ngemera alisema malengo yao ni kumwezesha kila mtu kuchagua njia ya uzazi wa mpango anayoihitaji hasa miongoni mwa vijana.

“ Vijana wanaweza kudhani kuwa huduma za uzazi wa mpango ni kwa ajili ya watu walio katika ndoa tu, lakini ni muhimu pia kwao ili kuzuia mimba zisizo takiwa kabla ya ndoa. Nawaomba vijana kuhamasika na kampeni yetu ya chagua maisha kwa kutumia uzazi wa mpango”,alifafanua.

Kwa upande wake Miss Marie Stopes 2014, Doreen Benne, alisema mimba ambazo hazijapangiliwa, huchangia takribani vifo 1,400 kila mwaka vitokanavyo na utoaji mimba usiosalama.

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali Mkoani Singida wakisikiliza huduma za uzazi wa  mpango.

Pia zinachangia mamia ya wasichana kufukuzwa shule kwa kuwa na mimba zisizotarajiwa.

Alisema hatari ya hizo au madhara hayo yanaweza kutokomezwa /kuzuiwa endapo kila mtu atazingatia kikamilifu uzazi wa mpango.

Shirika la Marie Stopes ambalo mwaka jana lilishafikia miaka 25 kufanya kazi nchini, linahudumia na kuchangia asilimia 25 ya huduma za uzazi wa mpango unaotekelezwa hapa nchini.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida Wilbard Marandu akikata utepe wakati wa kuzindua gari litakalotumika kutoa huduma za mkoba za uzazi wa mpango Mkoani Singida.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida Wilbard Marandu akizindua gari litakalotumika kutoa huduma za mkoba za uzazi wa mpango Mkoani Singid

MATUKIO YA KUSIKITISHA YALIYOTOKEA CHINI YA MH. RAISI JAKAYA M KIKWETE


TAREHE 05-01-2011
Police wawapiga risasi watu zaidi
ya 11 ktk maandamano ya
CHADEMA. Waua watu 3.
TAREHE_10-2011
Dk.Mwakyembe aenda India
kutibiwa kutokana na Kupewa
Sumu.PoliCCM walipotezea kisiasa.
TAREHE_02-2012
Shehe Ali khamis Kuuawa kwa
mapanga.
TAREHE 26-06-2012
Dr.Ulimboka akatekwa na kufanyiwa
unyama.
TAREHE 18-07-2012
Mv spice yazama.
TAREHE 02-09-2012
Daudi Mwangosi auliwa na polisi
Iringa.
TAREHE 28-09-2012
LHRC Waishtaki serikali ya K.. ICC
TAREHE 12-10-2012
Mtoto kudhihaki Kitabu kitakatifu
(haijawahi kutokea Tz)
TAREHE 16-10-2012
Shehe Farid A. Hadi kiongozi wa
Uhamsho kutekwa na kupotea
(Alipatikana)
TAREHE _12-2012
Padre Ambrose apigwa risasi
Zanzibar
TAREHE _02-2013
Padre Evarist Mushi apigwa risasi
Zanzibar.
TAREHE 18-02-2013
Matokeo kidato cha 4
mabovu,haijawahi kutokea duniani
tangu kuumbwa kwa Adam na
Hawa.
Waliopata div 4 na 0 ni takriban
95%
TAREHE 05-03-2013
Kibanda afanyiwa ya Ulimboka.
TAREHE _03-2013
Lwakatale (mkurugenzi wa usalama
CHADEMA) atuhumiwa kwa Ugaidi.
TAREHE 17-04-2013
wabunge 6 wa CHADEMA watolewa
nje ya bunge,Ndugai/naibu spika
awapa adhabu ya kutoingia
bungeni siku 5 kinyume na kanuni
za bunge.
Siku hiyohiyo mh.Lema amtaja Rais
kuwa ndie mwanzilishi wa udini.
TAREHE 25-04-2013
Lema avamiwa usiku wa manane
na polisi kwa amri ya Mulongo/
mkuu wa mkoa wa Arusha
UPDATE,
TAREHE 05-05-2013
Mlipuko watokea kanisani Arusha...
Mheshimiwa rais akiwa angani na
ndege kuelekea Kuwait kuta..
TAREHE 08-05-2013
Lwakatale/mkulugenzi wa usalama
wa CHADEMA afutiwa mashtaka ya
ugaidi.
MWAKA 2013
.Deni la taifa lafikia tril.22 wakati
Kikwete alikuta deni ni tril.5
.Dola moja=1,600 tshs wakat
alikuta dola moja=600tshs.
TAREHE 14-05-2013
tetesi za
Kikwete kuandaliwa mpango wa
kuwa rais wa Tz hadi mwaka 2017
badala ya mwaka 2015,ili asimamie
kukamilika kwa uundwaji wa katiba
mpya.
Source,Mh.Pro.Lipumba.
UPDATES:
TAREHE 18-05-2013
Tetesi: Kanisa la TAG ladaiwa
kuchomwa moto leo hii....
TAREHE 19-05-2013
Iringa, Police wawashambulia
Wamachinga kwa Mabomu ya
machozi kuwaondoa eneo
wanalofanyia kazi.
Mh.Mch.Msigwa Mbunge wa Iringa
Mjini akamatwa na Police.
Tare.20-05-2013 Mhe.Msigwa
atolewa Lupango kwa dhamana.
TAREHE 22-05-2013
Ukaidi wa Kikwete na waziri wake
wa nishati na madini wasababisha
vurugu Mtwara watu wakipinga
ujenz wa bomba la gesi kwenda
Dar.
Zaidi ya watu 6 wakiwemo Police
wauawa.
(kama kunanilichokisahau ama
kukosea nikumbusheni at)
mfano,Tarehe aliyosema hajui
kwanini Tz ni maskin,msongamano
wa magali dar ni ishara ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

MKUU WA KITUO CHA POLISI NJOMBE MlAKA 30 JELA KWA KUBAKA

Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilembula
Njombe Afungwa Jela Miaka 30
kwa kosa la Kumbaka Mahabusu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa
ya Njombe, imemhukumu aliyekuwa
mkuu wa kituo cha Polisi Ilembula
kifungo cha miaka 30 jela, baada
ya kukutwa na hatia ya kumbaka
mtuhumiwa aliyekuwa ndani ya
mahabusu.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu
Augustine Rwezile, baada ya
mshtakiwa huyo James Nyambenga
kukiri kosa hilo mahakamani,
ambapo mshakiwa huyo anadaiwa
kumtoa msichana huyo kwenye
chumba cha mahabusu alikokuwa
anashikiliwa na kumbaka.
Mwanamke huyo ambae ni
mhudumu wa bar alikuwa
anashikiliwa kwenye mahabusu ya
kituo hicho kwa tuhuma za
uzururaji.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu
Rwezile amesema ushahidi
uliotolewa na upande wa
mlalamikaji na vielelezo vya daktari
aliyempima msichana huyo viliweza
kuithibitishia Mahakama kuwa
mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Friday, 20 February 2015

LIFE AND EDUCATION

"African Education system has surprising outcomes. The smartest students pass with 1st Class and get admissions to medical and engineering schools. The 2nd Class students get MBAs and LLB’s to manage the First Class students. The 3rd Class students enter politics, and rule both 1st and 2nd Class students. The Failures join the army and control politicians who, if they are not happy with, they kick or kill them. Best of all.....
those who did not attend any school, become  witch doctors, and everybody follows them."

Wednesday, 18 February 2015

RAISI KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27

*Atengua uteuzi wa Ma-DC 12, awabadilisha vituo 64, awabakiza 42 kwenye vituo vyao vya zamani

RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya 12.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais  Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42.

Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred Mwakalebela anayeenda wilayaya Wanging’ombe.

Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali Kimiang’ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni), Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S. Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara (Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen Zelothe (Musoma).

Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack (Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally Mohamed (Serengeti).

Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).

Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri, kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya (Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias Goroi (Rorya).

(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA.

JUMATANO, FEBRUARI 18, 201

Saturday, 7 February 2015

Brand mpya ya pikipiki

Kwa maekezo zaidi cheki nasi hapa 
           0652 060 209