LOWASSA AONGOZA KURA ZA URAIS.
Shirika la New Deal Africa kupitia mtandao wake wa
Easypolls.com wanaendesha utafiti (opinion poll) kwa wagombea Urais nchini Tanzania waliojitokeza hadi sasa ambao ni Edward Lowassa wa (CHADEMA /UKAWA) na John Magufuli (CCM).
Hadi leo jioni matokeo ya mtandao huo yanaonesha kuwa uchaguzi ungefanyika leo Lowassa angeshinda kwa 64%, na Magufuli angefuatia kwa 31%, huku 5% ya wapiga kura wakiwa hawajaamua wampigie nani kati ya Lowassa na Magufuli.
Bila shaka hawa ni wale wanaosubiri wagombea wa vyama vingine wajitokeze. Kwa maana hiyo ni kwamba wagombea watakaojitokeza kupitia ACT, TADEA, CHAUSTA, na vyama vingine watagawana 05% ya hao "undecided".