Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli si msafi katika utendaji kazi wake kama inavyoelezwa kwa Watanzania.
Zitto alijenga hoja yake ya kumtuhumu Magufuli kuwa si msafi kwa kudai kuwa kuna Sh. bilioni 87/= “zimeibiwa” Wizara ya Ujenzi ambayo ndiyo anayoiongoza.
“Fedha hizi ni sehemu ya Sh. bilioni 252/= za miradi ya umeme, barabara na miradi maalumu zilizokosa maelezo yake kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ambapo kukosekana kwa fedha hizo ni kiashiria cha kuwapo matumizi mabaya katika wizara iliyoongozwa na Magufuli,’ alisema Zitto.

No comments:
Post a Comment