Thursday, 26 March 2015

KIKWETE ATEUA WABUNGE WAWILI WAPYA

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz              
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.

Rais amefanya uteuzi huu  kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.

Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa  kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.

Wabunge ambao wameshateuliwa ni:
Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
Mhe. Janet Zebedayo Mbene
Mhe. Saada Salum Mkuya
Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
Mhe. James Fransis Mbatia

Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi, 2015.

……………………………MWISHO……………………………….
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu-Dar-Es-Salaam
26 Machi, 2015

No comments:

Post a Comment