Imetimia, Makongoro Nyerere ndie chaguo rasmi la Kikwete urais.
Yericko Nyerere 11:38 Today
Wakuu,
Mtakumbuka wiki juzi niliwajuza kuwa rais Kikwete baada ya kuona ccm imekufa na hataki chama kizikwe mikononi mwake, aliomba ushauri kwa marais waastafu wa Afrika katika makutano yao kule Ethiopia. Walimshauri kua ajaribu kuokoa jahazi kwakukirudisha chama kwa familia ya mwasisi, Mama Maria Nyerere amajaribu kupinga suala hili lakini ameshindwa, washawishi hasa waandamizi wa dola wamekuwa na nguvu na hata vitisho.
Jana kulikuwa na kikao cha ukoo na wazee wa Musoma ili kupima na kuamua kumruhusu kijana wao mpendwa Makongoro Julius Nyerere kuwa ndie awe mrithi rasmi wa Kikwete.
Kikao hicho kimefanywa kwa ombi la rais Kikwete kwa wazee hao, ambapo wazee kwa kauli moja wamempa baraka zote kuwa kijana avae viatu vya marehemu Baba yake Mzee Julius Nyerere.
Baada ya jana kupata baraka zote, mda huu Makongoro amesafiri kutoka Musoma kuja Dar ambapo tayari ulinzi kwake umeimarishwa maradufu, sasa amepewa ulinzi ma nne ya aliokuwa nao hapo awali
No comments:
Post a Comment